Kitengo cha kusimamia haram kimegawa halwa (pipi) kwa mazuwaru katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Albaaqir na Alhaadi (a.s)

Kitengo cha kusimamia haram katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimegawa halwa (pipi) kwa mazuwaru kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Albaaqir na Alhaadi (a.s).

Makamo rais wa kitengo Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema, “Kwenye kila tukio la kuadhimisha mazazi matakatifu ya Ahlulbait (a.s) watumishi wa kitengo hugawa marashi, mauwa na halwa (pipi) kwa mazuwaru wa mwezi wa familia (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Hafla ya kwanza kufaywa katika mwezi huu ni kuadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s), Ataba tukufu imepambwa pamoja na barabara zinazoelekea kwenye Ataba katika maadhimisho haya matukufu”.

Atabatu Abbasiyya imefanya hafla kubwa ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s), kwenye uwanja wa mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kugawa zawadi kwa washindi wa shindano maalum lililofanywa kwa njia ya mtandao.

Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio ya kidini yanayohuisha utajo wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: