Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimetoa muhadhara kuhusu historia ya Imamu Muhammad Albaaqir (a.s).
Rais wa kitengo Shekhe Swalahu Karbalai amesema: “Kitengo cha Dini kimetoa muhadhara kuhusu historia ya Imamu Muhammad Albaaqir (a.s), ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mbele ya kundi kubwa la mazuwaru watukufu, muhadhara huo ni sehemu ya ratiba ya shughuli za kidini inayoendeshwa na kitengo katika mwezi mtukufu wa Rajabu, kwa lengo la kuhuisha utajo wa Ahlulbait (a.s) na kutangaza utukufu wao”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara umeeleza maudhui mbalimbali, miongoni mwake namna Imamu Albaaqir (a.s) alivyo pambana kufundisha watu ukweli na hukumu za kisheria”.
Akabainisha kuwa “Muhadhara umejikita katika kueleza zama za Imamu Albaaqir (a.s) na vitu muhimu vilivyotokea katika zama hizo, ikiwemo kuanzishwa kwa Hauza tukufu za kielimu (shule)”.




