Atabatu Abbasiyya inafanya shindano maalum la kitamaduni kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Aljawaad (a.s)

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza kufanyika kwa shindano la kitamaduni kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Majina ya washindi kumi yatatangazwa siku ya Alkhamisi (9/1/2025m) kwenye jukwaa la Atabatu Abbasiyya, sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) itakayofanywa kwenye uwanja wa mlango wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Ijumaa (10/1/2025m) sawa na (9 Rajabu 1446h) baada ya swala ya Magharibi na Isha.

Iwapo mshindi atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria kwenye hafla hiyo, atatakiwa kwenda kwenye ofisi za wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya siku nne (4) toka kutangazwa kwa matokeo, akiwa na nyaraka zinazo mthibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: