Makundi ya mazuwaru wanahuisha usiku wa Ijumaa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kuhuisha usiku wa Ijumaa mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mji wa Karbala hupokea idadi kubwa ya mazuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao huja kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).

Ziara hii inaenda sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa Imamu Muhammad Albaaqir na Ali Alhaadi (a.s), waliozaliwa siku za kwanza katika mwezi mtukufu wa Rajabu.

Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake, inafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: