Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhadi (a.s) katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Majlisi imesimamiwa na idara ya wahadhiri chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) na itadumu kwa muda wa siku tatu.
Mhadhiri wa Majlisi Shekhe Abduswahibu Asadi amesema “Atabatu Abbasiyya imeomboleza kifo cha Imamu Ali Alhadi (a.s) kilicho tokea mwezi tatu Rajabu, kwa kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Mawaidha yamejikita katika kumuelezea Imamu Alhaadi (a.s), historia yake, ukarimu wake, elimu yake pamoja na kueleza umuhimu wa kufanya mazingatio katika usomaji wa Qur’ani tukufu”.
Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio ya kidini na yale yanayohusu Ahlulbait (a.s), kwa lengo la kutambulisha elimu na utukufu wao katika kutumikia Dini na jamii.




