Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, zimeomboleza kifo cha Imamu Ali Alhaadi (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.
Mmoja wa watumishi wa idara ya Masayyid katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Badri Mamitha amesema “Watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wamefanya maukibu ya pamoja katika kuomboleza kifo cha Imamu Ali Alhaadi (a.s), wameimba qaswida na mashairi ya kuomboleza yaliyo amsha hisia za majonzi na huzuni katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Waombolezaji wamefanya matembezi kuanzia ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) kwenda kumpa pole kwa msiba huu mkubwa”, akasema kuwa, “Maukibu imehitimisha kwa kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s)”.
Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, hufanya maukibu ya pamoja katika kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).



























