Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amefanya kikao kilichohusisha baadhi ya viongozi wa kielimu kwa ajili ya kujadili maandalizi ya kuadhimisha (hauza ya Najafu Ashrafu) yanayotarajiwa kufanywa mwaka 1448h.
Sayyid Swafi amesisitiza umuhimu wa jambo hilo, kwani linaonyesha nafasi ya hauza tukufu, iliyotoa maelfu ya wasomi na watafiti wanaofanya kazi ya kufundisha uislamu na kutangaza madhehebu duniani.
Kikao kimeazimia kuwa na miradi tofauti ya kielimu, ikiwa ni pamoja na kufanya kongamano maalum la Shekhe Abu Jafari Tusi, kuandika kitabu kikubwa kuhusu athari ya hauza ya Najafu katika elimu tofauti, kama vile elimu ya Adida, Fiqhi, Usulu-Fiqhi, Lugha ya kiarabu na zinginezo, sambamba na kuandika historia ya matukio muhimu yaliyojiri katika mji huo na hauza yake namna ilivyo anzishwa.
Atabatu Abbasiyya imechukua jukumu la kuandaa hafla hiyo, kutokana na umuhimu wa kuhuisha turathi za kidini na utamaduni wa mji huo mtukufu pamoja na hauza yake katika taifa la Iraq na ulimwengu wa kiislamu kwa ujumla.

