Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza majina ya waliofuzu kwenye shindano la kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Masharti ya kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), itakayofanywa kwenye eneo la mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Ijumaa (10/01/2025m) baada ya swala ya Magharibi na Ishaa.
Iwapo atapata udhuru wa kushindwa kuhudhuria, atatakiwa kufika katika ofisi za wahasibu wa Ataba tukufu ndani ya muda usiozidi siku nne toka kutolewa kwa majibu hayo, akiwa na nyaraka zinazo mthibitisha (kitambulisho cha uraia au hati ya kusafiria.

