Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, kimejadili na hauza ya Qum takatifu, njia za kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uandishi, uhakiki na faharasi.
Majadiliano hayo yamefanywa baada ya ugeni kutoka hauza ya Qum, kutembelea kitengo cha maarifa, ambapo wamepokewa na rais wa kitengo hicho Shekhe Ammaar Hilali.
Wageni wamepewa maelezo kuhusu mafanikio ya kitengo na vituo vyake, pamoja na kuambiwa kwa ufupi kuhusu mikakati ya baadae.
Wakajadili njia za kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uandishi, uhakiki na faharasi pamoja na harakati zingine, kama vile kufanya makongamano, nadwa, vikao na warsha.



