Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamegawa haluwa (pipi) kwa mazuwaru, ikiwa kama ishara ya kuonyesha furaha kwa maadhimisho hayo matukufu, sambamba na kupamba malalo kwa mauwa na mabango.
Atabatu Abbasiyya huadhimisha matukio yote yanayohusu kumbukumbu za kuzaliwa kwa Ahlulbait (a.s), pamoja na kugawa marashi, mauwa na haluwa kwa mazuwaru wa mwezi wa familia (a.s).