Katibu mkuu wa Atabatu Askariyya amempongeza katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya kwa kuteuliwa tena katika nafasi hiyo

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amepokea ugeni kutoka Atabatu Askariyya ukiongozwa na katibu mkuu wake Dokta Naafii Jamiil.

Ugeni huo umetoa pongezi kwa Sayyid Aalu Dhiyaau-Dini kwa kuteuliwa tena kuwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya kwa miaka mingine mitatu, sambamba na kutoa pongezi kwa watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu, makamo katibu mkuu na marais wa vitengo, wakawatakia mafanikio mema katika kazi zote za kuwahudumia mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Uongozi wa Wakfu-Shia ulitoa tamko la kumteua Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini kuwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, tamko linasema:

Kutokana na msimamo wa Muheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, tarehe 13 Rabiul-Aakhar 1446h, na kwa mujibu wa kifungu namba (4) tatu/ cha kanuni za Wakfu-Shia namba (57) ya mwaka 2012, kutokana na faida za kiutendaji, tunamteua tena Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini kuwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa miaka mitatu mingine, kuanzia tarehe iliyokuwa unaishia uteuzi uliotangulia”.

Akaongeza kuwa “Sayyid Mustwafa Murtadha Abudi Aalu Dhiyaau-Dini, anajukumu la kumteua makamo katibu mkuu na wajumbe watano wa kamati kuu watakaofanya kazi pamoja nae”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: