Atabatu Abbasiyya tukufu, imeadhimisha mazazi ya Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) katika eneo la vitalu vya Alkafeel.
Kiongozi wa vitalu Sayyid Muhammad Harbi amesema “Miongoni mwa hafla zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya kwenye maeneo tofauti katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Aljawaad (a.s) ni hafla iliyofanywa kwenye vitalu vya Alkafeel”.
Akaongeza kuwa “Hafla imehudhuriwa na kundi kubwa la familia za watu wa Karbala, imepambwa na qaswida na tenzi”.
Akabainisha kuwa “Atabatu Abbaisiyya huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s)”.