Maukibu ya watu wa Karbala inaadhimisha mazazi ya Imamu Ali (a.s) mbele ya malalo yake takatifu

Maukibu ya watu wa Karbala imeadhimisha mazazi ya Imamu Ali (a.s) mbele ya malalo yake takatifu katika mkoa wa Najafu.

Mmoja wa watumishi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, Sayyid Haidari Ibrahim amesema “Watu wa Karbala wameadhimisha mazazi ya Imamu Ali (a.s) katika usiku wa mwezi 13 Rajabu mbele ya malalo takatifu na kuhuisha utiifu kwa kiongozi wa waumini (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa yanayohitajiwa na maukibu katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Ali (a.s), ikiwa ni pamoja na gari maalum za kubeba mazuwaru na kuimarisha usalama”.

Mmoja wa washiriki wa maukibu, Sayyid Khalid Ibrahim aesema, Maukibu imekuwa ikifanya maadhimisho haya ndani ya haram ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa mwaka wa kumi na tisa mfululizo. Akasema kuwa “Atabatu Abbasiyya imerahisisha shughuli za mawakibu na kuweka mazingira mazuri kwa mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: