Rais wa kitengo Sayyid Nasoro Hussein Mut’ibu amesema “Kitengo kimefanya majlisi ya kuadhimisha mazazi ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, imehudhuriwa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya na kundi kubwa la familia za watu wa Karbala”.
Akaongeza kuwa “Hafla ilikuwa na vipengele tofauti, kikiwemo kipengele cha qaswida na tenzi zinazoelezea mapenzi kwa Ahlulbait (s.a)”.
Akabainisha kuwa “Kitengo huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), kwa lengo la kusambaza mafundisho yao na kuhuisha mambo yao (a.s)”.