Kiongozi wa idara ya umeme Mhandisi Hassan Muhammad amesema “Watumishi wa idara wamebadilisha taa za ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya pamoja na zile zinazozunguka eneo la Ataba na kufunga nyekundu, kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Taa zilizobadilishwa ni zile nyeupe, kijani na za rangi zingine na kufungwa nyekundu, kwani taa nyekundu huendana na mazingira ya huzuni katika kuomboleza msiba huu mkubwa”.
Akafafanua kuwa “Jambo hili ni sehemu ya mpango kazi wa mwaka unaotekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, wa kuweka mazingira yanayo endana na matukio”.





