Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, inaomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).
Ratiba ya uombolezaji imefanywa kwa kushirikiana na kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s), imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na igizo lenye anuani isemayo (Jeraha la Sham), limeeleza baadhi ya mambo yanayomuhusu Bi Zainabu (a.s), kuanzia kuzaliwa kwake (a.s) hadi kifo chake.
Ratiba ikahitimishwa kwa kufanya majlisi ya kuomboleza, iliyopambwa na qaswida zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi, sambamba na kutoa pole kwa Imamu wa zama (a.f).
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi za kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), kwa lengo la kufundisha elimu yao na kueleza utukufu wao katika jamii.




