Atabatu Abbasiyya inaendelea kufanya majlisi za kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s)

Atabatu Abbasiyya inaendelea kufanya majlisi za kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Bibi Zainabu (a.s).

Majlisi hizo zinasimamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu.

Mhadhiri wa majlisi Shekhe Raadu Khatibu amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kundi la waumini”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umetaja baadhi ya vipengele katika historia ya Bibi Zainabu (a.s), ikiwemo elimu yake, ukarimu wake, kujitolea kwake na khutuba zake”.

Atabatu Abbasiyya hufanya maadhimisho yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kusambaza ujumbe wao na kufuata mwenendo wao mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: