Ameyasema hayo wakati akimpokea kiongozi wa idara ya watoto na makuzi kutoka kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Hasanain Faruq, ambaye ameeleza maudhui za kitabu chake kiitwacho (Nafasi ya Atabatu Abbasiyya katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu nchini Iraq mwaka 2017m).
Muheshimiwa amesisitiza kuwa Ataba tukufu itaendelea kusaidia watafiti na sekta ya elimu katika kuimarisha tafiti za kielimu na program zinazosaidia jamii, sambamba na kuandaa mazingira mazuri ya kubadilishana uzowefu baina ya watafiti na wabobezi wa sekta ya maendeleo endelevu.
Akaendelea kusisitiza umuhimu wa kuandika harakati za Ataba na miradi yake katika sekta ya elimu, afya, mazingira, huduma za umma, viwanda, kilimo na zinginezo na namna ambavyo imesaidia kuboresha maisha ya raia, akasema kuwa Ataba inafanya kila iwezalo katika kutatua changamoto za jamii.
Akapongeza kazi nzuri iliyofanywa na mtafiti ya kuandika harakati na miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na kubainisha nafasi ya miradi hiyo katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
Utafiti umeandika juhudi za Ataba tukufu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu na miradi mbalimbali ya kuhudumia jamii.


