Rais wa kitengo cha mgahawa (mudhifu) katika Atabatu Abbasiyya, Sayyid Aadil Hamami amesema kuwa, tumegawa zaidi ya sahani za chakula elfu 50 kwenye maombolezo ya kifo cha Bibi Zainabu (a.s) katika mji wa Karbala.
Akasema kuwa “Tumegawa chakula kwa muda wa siku nne, kila siku milo miwili mikuu, pamoja na ugawaji wa chakula chepesi kulingana na mahitaji ya mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Huduma hii ni sehemu ya jitihada za Ataba tukufu za kuhudumia watu wanaokuja kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati maalum wa kutoa huduma tofauti kulingana na mahitaji ya mazuwaru, miongoni mwa huduma hizo ni, kuimarisha ulinzi na usalama, utoaji wa huduma za afya, chakula na zinginezo, kwa lengo la kuweka mazingira salama na tulivu kiibada.







