Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa semina ya kuwajengea uwezo watimishi wa idara ya wanawake katika Ataba tukufu.
Mkuu wa kituo Bibi Sara Alhafaar amesema “Semina imesimamiwa na mshauri wa mafunzo kutoka kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu Sayyid Ali Shimri kwa muda wa siku tatu, kila siku wanasoma saa tatu”.
Akaongeza kuwa “Semina imehusu misingi ya protoka na umuhimu wake kuboresha mawasiliano ya kijamii ndani na nje ya mazingira ya kazi”.
Akasema “Semina hii ni sehemu ya kuboresha uwezo wa watumishi wa kike katika Ataba tukufu”.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya semina na warsha kwa watumishi wake ili kuwajengea uwezo na kuboresha utendaji wao.