Atabatu Abbasiyya imetoa zawadi kwa wanafunzi 250 wanaovaa Abaa sawa na ya Bibi Zainabu katika chuo kikuu cha Kirkuk, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya kongamano la Aqilah (a.s).
Kongamano linafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Kujistiri na hijabu) kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, chini ya kitengo cha mahusiano katika Ataba tukufu, kongamano limefanywa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kirkuk, katika kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).
Kongamano lilikuwa na vipengele vingi, kikiwemo cha kutoa zawadi kwa wanafunzi 250 ambao huvaa Abaa sawa na ya Bibi Zainabu katika mazingira ya chuo, sambamba na uwasilishwaji wa jumbe mbalimbali, miongoni mwa jumbe hizo ni: ujumbe kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, chuo kikuu cha Kirkuk, kipengele cha mashairi na tafiti za kielimu.
Atabatu Abbasiyya hufanya mikutano na makongamano mbalimbali ndani ya vyuo vikuu vya Iraq, kwa lengo la kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) na kuimarisha mafungamano ya wanafunzi na mwenendo wa Ahlulbait (a.s).