Mkuu wa kitengo cha maelekezo ya kinafsi na kimalezi katika chuo hicho Dokta Husam Ubaidi amesema “Chuo kimefanya kongamano lililopambwa na matukio mbalimbali, miongoni mwa matukio hayo ni: muhadhara elekezi kutoka kwa Sayyid Jafari Almuruji, ameongea kuhusu mazingatio na masomo yanayopatikana katika historia ya Ahlulbait (a.s), jinsi ya kunufaika na mafundisho hayo katika maisha ya kielimu na maonyesho ya kazi mbalimbali za kibunifu zilizofanywa na wanafunzi”.
Akaongeza kuwa “Chuo hutumia fursa ya kunufaika na matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) wakati wa kuadhimisha utajo wao mbele ya wanafunzi”.
Kupitia harakati hizi, chuo kinajenga kizazi cha vijana wanaojitambua na wenye maadili mema, na ndio lengo kuu la chuo lupitia ratiba za kimalezi, kwa mujibu wa maelezo ya Ubaidi.