Kitengo cha utalii wa kidini kimeratibu muhadhara elekezi kwa watu wanaokwenda kufanya Umra kupitia msafara wa Saaqi

Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya, kimeratibu muhadhara elekezi kwa watu wanaokwenda kufanya Umra kupitia (msafara wa Saaqi) katika mwaka 2025m.

Mmoja wa wahudumu wa kitengo Sayyid Abdullahi Karim amesema “Kitengo kimeratibu muhadhara elekezi wenye mafunzo ya kiidara na kidini, sambamba na kusherehesha ibada katika Masjid Nabawi na Masjid Haraam ya Maka kwa wenye kufanya Umra, ili kuwaandaa katika ufanyaji wa idara ya Umra”.

Akaongeza kuwa “Safari ya Umra inahusisha watu kutoka mikoa yote ya Iraq, wamekuja kujiandaa na ibada hiyo takatifu itakayofanywa katika mji wa Madina na Maka”.

Atabatu Abbasiyya hutoa huduma bora kwa mazuwaru wa Ataba takatifu na Mazaru tukufu pamoja na wanaokwenda kufanya ibada ya Umra kupitia (msafara wa Saaqi)
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: