Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimechapisha toleo la (182) la jarida la Riyahaini ambalo hutoka kila mwezi, linalolenga kujenga uwelewa wa watoto.
Kiongozi wa idara ya watoto na makuzi Sayyid Hasanaini Faruq amesema “Jarida la Riyahaini linaupekee wa kuandika maudhui mbalimbali kwenye mada tofauti, kama vile adabu, sayansi na zinginezo, kwa kiasi ambacho huibua hisia za watoto na kuwashajihisha kusoma”.
Akaongeza kuwa “Jarida limejikita katika kukuza uwezo wa watoto katika usomaji wa Qur’ani na kufanya tafakuri, jambo ambalo linasaidia kutengeneza kizazi cha watu wanaojitambua wenye uwezo wa kupambana na changamoto za kijamii”.
Jarida linapatikana kwenye vituo vya mauzo vilivyopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.



