Atabatu Abbasiyya imeanza kukarabati mto wa Hindiyya katika mji wa Karbala

Kiongozi wa kikundi cha vitalu vya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Harbi, amesema kuwa wameanza kufanya ukarabati wa mto wa Hindiyya katika mji wa Karbala, ikiwa ni sehemu ya kuitikia maombi ya watu wa mtaa wa Naqiib.

Amesema kuwa “Wakazi wa mtaa wa Naqiib katika mkoa wa Karbala, walipeleka maombi kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba tukufu, Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ya kuujali mto wa Hindiyya, kwani unahistoria kubwa inayotakiwa kulindwa na kuenziwa wakati wote”.

Akaongeza kuwa “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria, Tutaweka kamera za ulinzi, kutengeneza madaraja mapya na kudumisha usafi, ameelekeza kuunda kamati maalum itakayosimamia jambo hilo, akasisitiza kuwa lengo ni kuweka mto katika hali ya usafi wakati wote kwa namna ambayo inaendana na hadhi ya mji wa Karbala na kuwaridhisha wakazi wa eneo hilo”.

Akasema kuwa “Kuna mpango kazi kamili ambao tumekubaliana na wakazi wa eneo hilo, watumishi wa Ataba tukufu wamesha anza kuutekeleza, unahusisha kufanya usafi, kuweka zege kwenye kuta za mto, kuweka taa na kupanda miti mipya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: