Atabatu Abbasiyya inasimamia kongamano la mwaka kimataifa (Kumbukumbu ya maumivu ya Iraq), karne ya jinai, unyama na mauaji ya halaiki.
Kongamano linafanywa kwa kushirikiana baina ya kiti cha Unesco cha tafiti za kuzuwia mauaji ya halaiki katika chuo cha Adadu, kituo cha Iraq cha kuthibitisha jinai za magaidi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Ataba tukufu, taasisi ya Shuhadaa, taasisi ya wafungwa wa kisiasa na kamati kuu ya kitaifa ya uadilifu.
Kongamano litafanywa katika mji mtukufu wa Karbala siku ya tarehe 16 na 17 Aprili, litaangazia changamoto za kihistoria na jinai zilizofanywa Iraq, sambamba na kuangalia utatuzi wa changamoto hizo na jinsi ya kujenga mustakbali mwema utakaojaa amani na uadilifu.
