Kikosi cha Abbasi (a.s) kinahudumia mazuwaru katika mji wa Kadhimiyya

Kikosi cha Abbasi (a.s) kinahudumia mawakibu za mazuwaru wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika mnasaba wa kuomboleza kifo chake.

Kiongozi wa kikosi cha wahudumu Sayyid Hussein Aamir amesema “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Sayyid Maitham Zaidi, kikosi chetu kimeanza kuhudumia mazuwaru wa malalo ya Imamu Alkadhim (a.s) katika kuomboleza kifo chake”.

Akaongeza kuwa “Kikosi chetu kinagawa maelfu ya sahani za chakula kwa mazuwaru kila siku”, akasema “Tumetengeneza bekari maalum ya kuoka mikate, tunaoka zaidi ya mikate elfu 20 kila siku”.

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya katika mji wa Kadhimiyya unatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Imamu Mussa Bun Jafari Alkadhim (a.s), ikiwa ni pamoja na ugawaji wa chakula, huduma za afya, sehemu za kulala mazuwaru sambamba na kushirikiana na sekta zingine katika utoaji wa huduma tofauti ndani ya mji huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: