Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake chini ya ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya inaomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s) kupitia majlisi za kuomboleza.
Kiongozi wa Idara Bibi Taghrida Tamimi amesema “Idara imefanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s), ikiwemo majlisi iliyofanywa katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s), nyingine katika Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya na sehemu zingine mbalimbali kupitia mradi wa mawaidha mema”.
Akaongeza kuwa “Majlisi zimepambwa na igizo lenye anuani isemayo (Mhazini wa elimu ya mitume), limeonyesha sehemu ya maisha ya Imamu Alkadhim (a.s), ikiwemo sehemu ya Toba, njama za watawala wa Bani Abbasi dhidi yake, hadi kufikia kuuawa kwake (a.s) na namna alivyopewa sumu”.
Majlisi zimeandaliwa na kuendeshwa kwa kushirikiana na idara ya wasichana katika Atabatu Abbasiyya, katika kuomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s) na kuonyesha sehemu ya historia yake tukufu.




