Hafla imehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Dokta Abbasi Didah Mussawi, Dokta Afdhalu Shami na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Jawadi Hasanawi pamoja na viongozi wengine.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo katika Ataba tukufu Dokta Mushtaqu Ali amesema “Kikao cha usomaji wa Qur’ani kimefanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuadhimisha kupewa Utume mtukufu na siku ya kimataifa ya Qur’ani”.
Akaongeza kuwa “Hafla imehudhuriwa na wasomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wasomaji wa ndani na nje ya Iraq, inalenga kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa mazuwaru watukufu”.
Atabatu Abbasiyya hufanya hafla za usomaji wa Qur’ani katika kuadhimisha kumbukumbu ya kupewa Utume mwezi ishirini na saba Rajabu.

















