Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wanawapongeza mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kupewa utume mtukufu (Mab’ath-Nnabawi).
Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Abidina Quraish amesema “Wahudumu wa kitengo wameweka mazingira ya furaha kwa kupanga maua, mabango na kugawa halwa (pipi), kufuatia tukio la kumbukumbu ya kupewa Utume mtukufu”.
Akaongeza kuwa “Ataba tukufu kwenye kila tukio linalohusu Ahlulbait (a.s) huweka maua, mabango na kugawa halwa kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akasema kuwa “Lengo la kuhuisha matukio haya katika Atabatu Abbasiyya ni kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s) na kuzingatia mafundisho yao matukufu sambamba na kushikamana na kizazi kitakatifu”.




