Kongamano la Saqaa la Qur’ani tukufu awamu ya nne, lililoandaliwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya limetoa zawadi kwa mahafidh 29 wa Qur’ani tukufu.
Vimetolewa vyeti vya ushiriki na zawadi kwa mahafidh, kutokana na juhudi zao za kukamilisha kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Utoaji wa zawadi ni sehemu ya kuonyesha kujali mahafidh na kushajihisha wanafunzi wengine waongeze juhudi katika kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.
Kongamano limehudhuriwa na idadi kubwa ya wasichana wakiwemo wawakilishi wa taasisi za Qur’ani, watafiti wa mambo yanayohusu Qur’ani na watumishi wa idara za wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu.