Ugeni kutoka muungano wa idhaa za nchi za kiarabu umetembelea Atabatu Abbasiyya na kuangalia huduma zinazotolewa kwa mazuwaru

Ugeni kutoka muungano wa idhaa za nchi za kiarabu, umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia huduma zinazotolewa kwa mazuwaru.

Ugeni huo umepokewa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba tukufu Sayyid Jawadi Hasanawi na baadhi ya viongozi.

Kiongozi mkuu wa muungano huo Sayyid Abdurahim Suleiman amesema “Tumetembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kupata nafasi ya kuongea na viongozi wa Ataba tukufu, tumesikiliza kwa makini historia ya malalo takatifu”.

Akaongeza kuwa “Tumeangalia huduma zinazotolewa kwa mamilioni ya mazuwaru wanaokuja katika mji wa Karbala kuzuru malalo tukufu”.

Atabatu Abbasiyya inaendelea kupokea wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Iraq, na kuwaonyesha kazi kubwa inayofanywa katika kuhudumia jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: