Makamo rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Ibrahim Tamimi amesema: “Kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa, kimefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani ya kimataifa kwa ushiriki wa wasomaji wengi wa ndani na nje ya Iraq”.
Akaongeza kuwa “Hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), nayo ni sehemu ya kuhuisha siku ya kimataifa ya Qur’ani tukufu”.
Majmaa-Ilmi hufanya matukio mengi yanayohusu Qur’ani katika kuadhimisha siku ya kitaifa ya Qur’ani tukufu.








