Atabatu Abbasiyya imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s)

Atabatu Abbasiyya imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya mjume wa kamati kuu Dokta Afdhalu Shami, mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Jawadi Hasanawi, baadhi ya viongozi wa Ataba, viongozi wa Dini na kundi kubwa la mazuwaru waliokuja kuadhimisha tukio hilo.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha Dokta Afdhalu Shami akawasilisha ujumbe wa katibu mkuu wa Ataba tukufu, ametoa pongezi kwa wahudhuriaji na umma wa kiislamu kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s).

Dokta Shami ameeleza historia ya Imamu Hussein (a.s), akafafanua nafasi yake mbele ya Mtume (s.a.w.w) na katika kusimamia misingi ya uadilifu.

Mjumbe wa kamati ya maadhimisho hayo katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqili Yasiri amesema “Hafla ilikua na vipengele vingi, miongoni mwake ni: Uwasilishaji wa ujumbe maalum wa maadhimisho, usomaji wa qaswida na mashairi sambamba na utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la (Swahaba Habibu bun Mudhwahir), kwa muandishi bora wa wafuasi wa Imamu Hussein (a.s), lililokua na washiriki wengi na kuchaguliwa washindi watatu”.

Akaongeza kuwa “Hafla imehitimishwa kwa kuwapa zawadi washindi wa shindano lililoandaliwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kufuatia mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s) ambapo jumla ya washindi kumi wa mwanzo wamepewa zawadi”

Atabatu Abbasiyya tukufu huadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s), ikiwa ni sehemu ya kujenga utamaduni bora wa kidini kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: