Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umewapongeza watumishi wa malalo ya Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya, umewapongeza watumishi wa malalo ya Imamu Hussein (a.s) katika kumbukumbu tukufu ya kuzaliwa kweke.

Ugeni umeongozwa na mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu Sayyid Muhammad Ashiqar, kwa ushiriki wa mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Jawadi Hasanawi pamoja na kundi kubwa la wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Sayyid Badri Mamitha mmoja wa wajumbe wa ugeni huo amesema: “Uongozi mkuu wa Ataba tukufu hutoa salamu za pongezi kwa watumishi wa malalo ya Imamu Hussein (a.s) kila mwaka, wakati wa kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake mwezi tatu Shabani”.

Akaongeza kuwa “Msafara wa ugeni huo umeanzia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwenda kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) ukiwa umebeba shada za maua huku wakiimba qaswida na tenzi zinazo ashiria furaha kubwa iliyojaa katika nyoyo zao, kwa ushiriki wa kundi la mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: