Wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya tukio la kiibada katika kuadhimisha mazazi yake

Wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya tukio la kiibada katika kuadhimisha mazazi ya tarehe nne Shabani.

Tukio hilo limehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, makamo wake Sayyid Abbasi Mussawi Ahmadi, wajumbe wa kamati kuu Sayyid Liith Mussawi, Dokta Abbasi Didah Mussawi, Dokta Afdhalu Shami pamoja na baadhi ya marais na viongozi wa vitengo.

Sayyid Liith Mussawi amesema “Watumishi wa malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya kitendo cha kiibada ndani ya malalo tukufu katika kuadhimisha mazazi hayo takatifu”,

Akaongeza kuwa “Wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) husimama mbele ya malalo tukufu kuhuisha ahadi na utiifu wao kwake wakati wa kuadhimisha matukio matukufu”.

Tukio la kiibada hufanywa kila siku ya Jumanne na Alkhamisi kila wiki, hufunguliwa kwa kusoma ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na watumishi wa malalo takatifu wakiwa wamesimama kwa mistari mbele ya kaburi tukufu, hufuatiwa na wimbo wa (Lahnul-Ibaa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: