Kituo cha utamaduni wa familia kimeratibu program ya kitamaduni kwa watumishi wa taasisi ya wafungwa wa kisiasa jijini Baghdad

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa program yenye anuani isemayo (Ishi kwa ubunifu) inayolenga watumishi wa kike katika taasisi ya wafungwa wa kisiasa kwenye mji mkuu wa Baghdad pamoja na wafungwa wa kisiasa katika mkoa wa Diyala.

Program ilikuwa na mihadhara miwili: wa kwanza ulikuwa na anuani isemayo (Familia ni ngome ya jamii) umewasilishwa na Dokta Maryam Abdulhussein, ameongea nafasi ya familia katika kujenga jamii yenye mshikamano kupitia misingi bora, muhadhara mwingine ukawa na anuani isemayo (Vituo vya kifikra) umewasilishwa na Bibi Sundusi Muhammad, ameeleza umuhimu wa fikra na jinsi ya kuzielekeza katika hatua za kumjenga mtu.

Program imejikita katika kuangalia misingi ya maisha bora katika jamii na namna ya kuwa mbunifu, kwa kuangalia mambo mbalimbali yanayo muhusu mwanamke.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: