Muwakilishi wa waziri wa mafuta ameangalia miradi ya Atabatu Abbasiyya na kapongeza huduma zake

Muwakilishi wa waziri wa mafuta Muheshimiwa Adnani Muhammad Hamudi ametembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Amefanya hivyo alipo tembelea Atabatu Abbasiyya akiwa na ujumbe uliohusisha katibu mkuu wa idara ya ufundi Sayyid Hasanaini Abdulatifu, mkuu wa kiwanda cha usafishaji wa mafuta katika mji wa Karbala Sayyid Haidari Sharifu, wamepokewa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Ataba tukufu Sayyid Jawadi Hasanawi, mkuu wa shirika la uzalishaji Alkafeel Sayyid Jafari Qutbi na baadhi ya viongozi wa Ataba.

Muwakilishi wa waziri na ujumbe aliofuatana nao wameangalia miradi kadhaa ya Atabatu Abbasiyya na kusikiliza maelezo kuhusu utendaji wa miradi hiyo.

Amepongeza miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya na huduma zinazotolewa kwa mazuwaru, na umuhimu wa miradi hiyo katika sekta ya utoaji wa huduma, viwanda na elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: