Rais wa chuo Dokta Nusir Shahidi Dahani amesema “Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya maadhimisho ya wahitimu wa awamu ya tano ya wanafunzi wa famasiya, sambamba na kutunukiwa hati ya kuaminika cha miaka mitano kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu na kuwa chuo cha kwanza kupata hati hiyo”.
Akaongeza kuwa “Maadhimisho hayo yanatokana na juhudi za wanafunzi wanaohitimu masomo yao kwa mafanikio na kwenda kuwa msaada mkubwa katika jamii, wakiwa na ujumbe wa elimu na ujuzi wa kuhudumia watu baada ya kuchota elimu katika kitivo cha famasiya kwenye chuo kikuu cha Alkafeel”.
Mkuu wa kitivo Dokta Saadi Mashkuri amesema “Tumefanya mahafali ya wahitimu wa awamu ya tano wa kitivo cha famasiya, wanaoenda kufanya majukumu yao ya afya katika jamii”.
























