Kiongozi wa haram tukufu Sayyid Muhammad Iswamu amesema “Semina imeandaliwa na kitengo cha Maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu tukufu kwa lengo la kuimarisha mazingira ya kirohi kwa watumishi na kuwaandaa kupokea mamilioni ya mazuwaru, semina itadumu kwa muda wa siku mbili”.
Muwezeshaji wa semina Shekhe Muhammad Jafari Twabsi amesema “Semina ni muhimu sana kwa washiriki, hueleza mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuamiliana na zaairu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuweka picha chanya ya huduma za malalo takatifu”.
Atabatu Abbasiyya hufanya semina na warsha mbalimbali zinazo lenga kuwajenga kiroho watumishi wake ili waweze kutoa huduma bora kwa mazuwaru.







