Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kielimu na kimataifa cha wiki ya Imamu wa tatu.
Mjumbe wa kamati ya elimu Dokta Twariq Ameedi amesema “Kikao kimegawa majukumu ya kielimu na kiidara sambamba na kuendeleza vikao vya ufafanuzi wa majukumu kwa kina”
Akaongeza kuwa “Inatarajiwa kuadhimishwa wiki ya Imamu kila mwaka sambamba na maadhimisho ya Idul-Ghadiir, ambapo hufanywa vikao vya kielimu asubuhi na jioni kwa idadi ya Maimamu watakasifu (a.s)”.
Akataja kuwa “Tumewasiliana na wasomi kutoka nje ya Iraq na tumefanya mazungumzo ya awali kuhusu ushiriki wao, tutafikia makubaliano ya mwisho na kubaini idadi na mada zitakazo wasilishwa baadae”.
Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi kubwa ya kusambaza elimu ya Ahlulbait (a.s) na historia yao pamoja na kubainisha nafasi yao katika kutatua changamoto na fikra potofu.



