Idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya inafanya maandalizi maalum ya kupokea mazuwaru wakati wa ziara tukufu ya Shaabaniyya.
Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hashim Shami amesema “Idara ya Masayyid imefaya kikao cha kujadili maandalizi ya kupokea mazuwaru katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani”.
Akaongeza kuwa “Kikao kimejadili mbinu za utoaji wa huduma bora kwa mazuwaru na kuandaa mahitaji ya lazima ili kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji wa ziara hiyo tukufu”.
Idara ya masayyid hufanya kila kitu kwa ajili ya kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika matukio ya kidini na ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu.



