Kitengo cha kulinda nidham kimeweka mkakati maalum wa ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani

Kitengo cha kulinda nidham katika Atabatu Abbasiyya, kimeanza kutekeleza mkakati maalum wa kuhuisha ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani.

Makamo rais wa kitengo Bibi Ridhwa Naaji amesema “Watumishi wa kitengo hujiandaa kuhudumia mamilioni ya mazuwaru katika ziara ya Shaabaniyya ambao huja kutoka kila sehemu ya dunia”.

Akaogeza kuwa “Kitengo kimeanza kuweka vizuwizi kwenye barabara zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuanzia barabara ya Maitham Tamaar, kupitia mlango wa Qibla, barabara ya Alqami, Hauraa Zainabu (a.s) sambamba na kuweka plastiki ndani ya haram tukufu kwa ajili ya harakati za mazuwaru”.

Akasema kuwa “Watumishi wa kitengo wanatumia mitambo ya kisasa zaidi iliyowekwa kwenye barabara zinazoelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mazuwaru watukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: