Njia zinazoelekea katika mji wa Karbala zimefurika watu wanaotembea kwa miguu kwenda kuhuisha ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ambayo hufanywa na waumini katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f) ni moja ya ziara ambayo huhudhuriwa na mamilioni ya watu katika mji wa Karbala kutoka ndani na nje ya Iraq.
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanafanya kila wawezalo katika kuhudumia mazuwaru watukufu.










