Idara ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya imetoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa kike wa nusu ya mwezi mtukufu wa Shabani.
Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya Bibi Mina Waaili amesema “Kutokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, imeandaliwa Sardabu maalum ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kutoa huduma kwa mazuwaru wa kike waliokuja kuhuisha usiku wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Huduma zimehusu sekta tofauti, miongoni mwake ni sekta ya afya, kwa kufungua vituo vya utoaji wa huduma ya kwanza, kuandaa sehemu maalum za kupumzika na sehemu za kufanyia ibada mbalimbali sambamba na kusimamia misafara ya kuingia na kutoka”.
Akasema kuwa “Huduma zinazotolewa na idara ya wanawake zinajumuisha mambo mengi, kwa kuzingatia malengo ya ziara na kuhakikisha yanafikiwa kwa usahihi”.






