Makundi ya mazuwaru wanahuisha usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani mbele ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) katika mji wa Karbala

Makundi ya mazuwaru wamehuisha usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani mbele ya Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s) katika mji mtukufu wa Karbala.

Mji wa Karbala umeshuhudia makundi makubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq waliokuja kufanya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani na kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).

Mazuwaru wanafanya ibada ya ziara na dua katika mazingira ya kiroho yaliyojaa amani na utulivu huku kukiwa na usimamizi mzuri wa misafara inayoingia na kutoka katika eneo la Maqaam tukufu.

Atabatu Abbasiyya inatoa huduma tofauti kwa mazuwaru, ikiwa ni pamoja na kuandaa sehemu ya kupumzika, chakula na utoaji wa huduma za matibabu bila kusahau uratibu wa ibada maalum zinazoendana na tukio hili tukufu.

Usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani ni miongoni mwa madukio muhimu kidini, waumini hukesha wakisoma dua na kuswali, sambamba na kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: