Kitengo cha uhusiano kimefanya warsha kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Qadisiyya

Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kimefanya warsha kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Qadisiyya.

Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule Sayyid Mahir Khalid amesema “Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya warsha yenye anuani isemayo (Mambo matano ya mtu mwenye mafanikio na kujitambua) kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Qadisiyya”.

Akaongeza kuwa “Warsha imetaja mambo mengi, miongoni mwake ni mikakati, mawasiliano, fikra chanya, matumizi ya muda, namna ya kujenga kipaji na mengineyo”, warsha imeshuhudia majadiliano mazuri na mwitikio mkubwa kutoka kwa washiriki.

Warsha imefanywa pembezoni mwa kongamano la (Watukufu waliozaliwa katika mwezi huu awamu ya tatu) linalo simamiwa na Ataba tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Qadisiyya, ili kujenga uwezo wa wanafunzi na vipaji vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: