Makamo katibu mkuu ameangalia maandalizi ya Mujammaa Abulfadhil Abbasi (a.s) uliopo barabara ya Najafu-Karbala, ya kupokea washiriki wa mahafali hiyo ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu vya Iraq na kutoka nchi za kiislamu (kikosi cha mabinti wa Alkafeel).
Maandalizi hayo yamehusisha uandaaji wa kumbi kubwa za kulala, ugawaji wa chakula, kuandaa vyoo, kutandika mazulia, kuandaa jukwaa kuu, kufunga vipaza sauti na kuweka vioo vya tv ukumbini.
Mahafali hiyo itafanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Kutokana na nuru ya Fatuma –a.s- tunaangazia ulimwengu) na anuani isemayo (kikosi cha mabinti wa Alkafeel awamu ya nane) tarehe 20 Februari (mwezi huu).
Mahafali hiyo huandaliwa na idara ya shuke za kidini Alkafeel, kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi 4000 kutoka mikoa tofauti ya Iraq na nchi za kiislamu.












