Kiongozi wa idara ya mafunzo katika kituo cha habari chini ya kitengo Sayyid Ali Fadhil amesema “Kituo kimeandaa semina ya kisasa katika sekta ya uhariri wa habari, kwa ushiriki wa wanahabari kutoka vitengo tofauti, itadumu kwa muda wa siku nne”.
Akaongeza kuwa “Semina imejikita katika kutambulisha vifaa vya kisasa katika uandishi wa habari kwa washiriki, jambo hilo ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya unaolenga kukuza uwezo wa waandishi wa habari na kuwafanya waendane na maendelea ya sekta hiyo”.
Mkufunzi wa semina Dokta Naji Nasiro amesema “Semina hii inaumuhimu maalum sambamba na ukuwaji wa teknolojia ya habari, mitandao ya mawasiliano ya kijamii ambayo imekua na athari kubwa katika sekta ya habari”.
Akabainisha kuwa “Watumishi wa sekta ya habari kuwapa semina kama hizi ni jambo muhimu, ili kujua mabadiliko yanayotokea katika sekta hiyo kimataifa”.
Akafafanua kuwa “Maendeleo ya teknolojia na mabadiliko ya njia za mawasiliano yanatutaka kusoma kwa umakini njia bora ya kutumia kufikisha ujumbe kwa walimwengu”.



