Kuhitimisha mafunzo maalum ya ushiriki kwenye mahafali ya wahitimu ya mabinti wa Alkafeel

Idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya imekamilisha mafunzo maalum ya ushiriki wa mahafali ya wahitimu ya (Mabinti wa Alkafeel) awamu ya nane.

Mtu wa kitengo cha ufundi katika mahafali hiyo Sayyid Ahmadi Risaam amesema “Leo tumekamilisha mafunzo maalum ya ushiriki wa ratiba za mahafali katika mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na shule za Al-Ameed”.

Akaongeza kuwa “Wanafunzi watasimama kwa mistari wakati wa matembezi yao, ili kuweka mfumo mzuri na mpangilio bora wa mahafali hiyo”.

Mahafali inasimamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Kutokana na nuru ya Fatuma –a.s- tunaangaza dunia) awamu ya nane ya mwaka wa masomo 2023/2024 kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi 4000 kutoka mikoa tofauti ya Iraq na nchi za kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: